Bara la Afrika sasa lina anwani yake
ya mtandao .africa sawa na ule wa .com kufuatia uzinduzi wake rasmi na
muungano wa Afrika AU.
Mwenyekiti wa tume ya umoja huo Nkoszana
Dlamini alipongeza uzinduzi wake kama wakati ambapo Afrika imejipatia
utambulisho wake wa kidijitali.AU inasema kuwa anwani ya .africa utalileta pamoja bara la Afrika kama jamii ya mtandao.
Anwani hiyo sasa itaonyesha maslahi ya makampuni barani Afrika.
Kwa mfano kampuni ya simu inaweza kuanzisha anwani yake ya mobile.africa ili kuonyesha uwepo wake barani Afrika.
Icann, kampuni inayotengeza anwani hizo iliiidhinisha hatua hiyo baada ya AU kuwasilisha ombi.
Kampuni hiyo iliongozwa na kampuni ya Afrika Kusini ZA Central Registry ambayo itahusika na usajili wa majina ya .africa.
No comments:
Post a Comment