• MISEMO

    Wednesday, March 5, 2014

    Israel yaikamata meli ya Iran iliyobeba silaha nzito

    Israel yaikamata meli ya Iran iliyobeba silaha.

    Israel imesema jeshi lake la baharini limeikamata meli ya Iran katika bahari ya Sham, ambayo ilikuwa ikisafirisha maroketi ya kisasa kwa kundi kipalestina la Hamas linaloudhibiti Ukanda wa Gaza. Msemaji wa jeshi la Israel amesema maroketi hayo ni aina ya M-302 yaliyotengenezwa nchini Syria, ambayo yanaweza kupiga shabaha iliyo umbali wa km 160.
    Msemaji huyo amesema maroketi hayo yangeiimarisha Hamas kwa kuipa uwezo wa kupiga maeneo karibu yote ndani ya Israel. Meli hiyo ilikuwa ikipeperusha bendera ya Panama, kituo chake cha mwisho kikiwa Port Said nchini Sudan.
    Meli za kivita za Israel zinaisindikiza meli hiyo yenye silaha ambayo imebadilishiwa njia na kuelekezwa kwenye bandari ya Eilat nchini Israel. Taarifa za jeshi la Israel zinaeleza kuwa mashirika ya kijasusi ya nchi hiyo yamekuwa yakiifuatilia meli hiyo kwa miezi kadhaa.

    No comments:

    Post a Comment

    Fashion

    Beauty

    Culture