• MISEMO

    Thursday, February 27, 2014

    WAZO LA DIAMOND


    WAZO LA DIAMOND

    Staa wa Bongo Fleva,Naseeb Abdul’Diamond Platinumz’amewachana wasanii wenzake wanaotafuta bifu na yeye na kusema kuwa amesikitishwa na baadhi ya wasanii wanaolazimisha kutengezeza ugomvi kilazima bila sababu za msingi.Kupitia account yake ya Instagram Diamond aliandika kuwa…kiukweli, nasikitishwa sana jinsi baadhi ya wasanii kutwa wanavyolazimisha kunitengenezea ugomvi wa kilazima pasipo kuwa na sababu… Aidha aliongeza kuwa kuna wasanii wengine wamekuwa wakisema kuwa amewatusi kwenye Media, Mara amepost kuwakashifu..

    Alimalizia kwa kusema kuwa yaani ilimradi tu....kwanini Wanamuziki wa Tanzania Tunashindwa kubadilika... mbona mi nahangaika na muziki wangu kimpango wangu... Mnasema nyie ndio mnaojua kuimba mie sijui "sinatatizo"... Mnasema nyie ndio wenye sauti nzuri yangu mbaya "Sina tatizo"... sasa mbona tena bado mnanifatilia na kutokujua kwangu... Nafkiri ni vyema mkaanza kutumia ujuzi wenu kukuza sanaa ya nchi yetu na kuleta heshima na maendeleo nchini, kuliko kupika majungu..... Watu wanataka kazi!Alimalizia kuandika kwenye Instagram

    No comments:

    Post a Comment

    Fashion

    Beauty

    Culture