• MISEMO

    Thursday, September 8, 2016

    NAJUA UNGEPENDA KUMJUA MZEE WA MIAKA 145 KUTOKA INDONESIA



    Mzee wa umri wa miaka 145 Indonesia


     chanzo bbc swahili

    Mzee wa umri wa miaka 145 Indonesia


    Mzee huyu kwa jina Mbah Ghoto kutoka Indonesia anaamini ndiye binadamu mzee zaidi kuwahi kuishi duniani.Anasema ameishi muda zaidi kushinda...................................
    wake zake wanne, ndugu zake 10 na wanawe wote.Anatokea kisiwa cha Java ya Kati."Huwa najaribu kuwa mvumilivu na kuamini kuwa kuna watu watakaonitunza," ameambia BBC."Nimeishi muda mrefu kwa sababu nina watu wanaonipenda na kunitunza."Yeye bado huvuta sigara.Mjukuu wake Suryanto anasema kwa mujibu wa stakabadhi rasmi za serikali, Mbah Gotho ana miaka 145. Alizaliwa 31 Desemba 1870."Tunaamini stakabadhi hizi ni halali, kwa mujibu wa nyaraka rasmi za serikali. Tunaamini tarehe yake ya kuzaliwa ni sahihi," anasema afisa wa serikali Wahyu Wiyanto.
    Indonesia ilianza kunakili rasmi kuzaliwa kwa watu 1900 hivyo ni vigumu kuthibitisha tarehe kamili ya watu waliozaliwa kabla ya hapo.
    Na kumewahi kutokea makosa awali.
    Lakini Mbah Gotho anachukuliwa kama shujaa eneo analotoka.
    "Siku ya Uhuru alikuwa akialikwa kusimulia yaliyotokea wakati wa vita. Anaweza kusimulia kuhusu vita dhidi ya wakoloni kutoka Japan na Uholanzi," anasema Wahyu Wiyanto.
    Mjukuu wake anasema mzee huyo huwa hana masharti mengi na huwa haitishi chakula maalum.
    "Kitu pekee alitutaka tufanye ni kununua jiwe la kaburi lake," anasema.
    Mzee huyo anasema kwa sasa anaishiwa na nguvu na hawezi kutarajia aishi muda mrefu zaidi.
    "Sina nguvu kama zamani. Hata kutembea ni shida. Nilikuwa mkulima na nilivua samaki mtoni. Sitaki kuendelea kuishi sana, ndio maana nimeandaa kaburi. "Ili nikifariki, kila kitu kiwe tayari," anasema.
    "Kwa sasa nataka tu kufariki, lakini wakati wangu haujafika bado."
    Mtu ambaye aliishi miaka mingi zaidi duniani kulingana na Guinness ni Jeanne Calment kutoka ufaransa ambaye aliishi miaka 122 na siku 164 . Aliaga dunia mwezi Agosti mwaka 1997.

    No comments:

    Post a Comment

    Fashion

    Beauty

    Culture