• MISEMO

    Friday, January 6, 2017

    Hollywood yabadilishwa kuwa ''Hollyweed'

    Hollywood yabadilishwa kuwa ''Hollyweed'

    Raia wa Los Angeles ambao ndio majirani wa eneo la kuigiza filamu maarufu 'Hollywood' waliamka mwaka mpya na kuona kwamba ubao wa ishara ya eneo hilo maarufu umebadilishwa na kuwa 'Hollyweed'.
    Vyombo vya habari katika eneo hilo vimeripoti kwamba maafisa wanalichukulia swala hilo kuwa dogo na kwamba wanaendelea na uchunguzi.
    Ishara hiyo ilioko katika mlima Lee ina herufi zenye urefu wa futi 45.
    Wapiga kura mjini California waliidhinisha sheria ya kuhalalisha bangi katika kura iliofanyika wakati mmoja na uchaguzi wa Marekani mnamo tarehe 8 Novemba.
    Mzaha huo hatahivyo haujaharibu herufi za ishara hiyo kwa kuwa herufi 'O' zilifanywa na kuwa 'E.'
    Gazeti la Los Angeles Times limeripoti kwamba mtu mmoja alirekodiwa akipanda katika ishara hiyo ili kubadilisha herufi hizo.
    Mzaha kama huo ulifanyika mnamo mwaka 1976 ili kulegeza sheria dhidi ya bangi.

    No comments:

    Post a Comment

    Fashion

    Beauty

    Culture