STAA wa fi lamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameeleza kukerwa na
mwanamuziki chipukizi, Athuman Omary ‘Harmorapa’ aliyesema amewahi
kutoka naye kimapenzi jambo ambalo siyo kweli.
Akichonga na Mikito Nusunusu Wolper alisema mwanamuziki huyo ambaye
ameimba kwenye wimbo wake wa Kiboko ya Mabishoo kuwa ameshatoka naye
kimapenzi amemkosea heshima na hata alivyousikia wimbo huo umemshangaza
kwa sababu hata Harmorapa mwenyewe anamuona kwenye mitandao ya kijamii
na magazetini tu hajawahi kumuona ‘live’.
“Jamani huku ni kukoseana heshima maana huyo Harmorapa hata simfahamu
huwa namuona kwenye mitandao na magazetini tu, sasa alivyoimba ametoka
na mimi kimapenzi naona kama ni kituko kikubwa sana,” alisema Wolper.
Fascinating!!!
ReplyDelete